1 Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,Kuliko mpotofu wa midomo aliye mpumbavu.
2 Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa;Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.
3 Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake;Na moyo wake hununa juu ya BWANA.
4 Utajiri huongeza rafiki wengi;Bali maskini hutengwa na rafiki yake.