11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake;Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
12 Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
13 Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye;Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.
14 Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
15 Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;Na nafsi yake mvivu itaona njaa.
16 Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake;Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA;Naye atamlipa kwa tendo lake jema.