14 Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
15 Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;Na nafsi yake mvivu itaona njaa.
16 Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake;Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA;Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
18 Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini;Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
19 Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake,Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena.
20 Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho,Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.