16 Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake;Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA;Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
18 Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini;Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
19 Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake,Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena.
20 Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho,Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.
21 Mna hila nyingi moyoni mwa mtu;Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.
22 Haja ya mwanadamu ni hisani yake;Ni afadhali maskini kuliko mwongo.