2 Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa;Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.
3 Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake;Na moyo wake hununa juu ya BWANA.
4 Utajiri huongeza rafiki wengi;Bali maskini hutengwa na rafiki yake.
5 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;Wala asemaye uongo hataokoka.
6 Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili;Na kila mtu ni rafiki yake atoaye tunu.
7 Ndugu zote wa maskini humchukia;Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye!Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.
8 Apataye hekima hujipenda nafsi yake;Ashikaye ufahamu atapata mema.