5 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;Wala asemaye uongo hataokoka.
6 Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili;Na kila mtu ni rafiki yake atoaye tunu.
7 Ndugu zote wa maskini humchukia;Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye!Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.
8 Apataye hekima hujipenda nafsi yake;Ashikaye ufahamu atapata mema.
9 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;Naye asemaye uongo ataangamia.
10 Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu;Sembuse mtumwa awatawale wakuu.
11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake;Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.