1 Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu,Na kuyaweka akiba maagizo yangu;
2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima,Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;
3 Naam, ukiita busara,Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4 Ukiutafuta kama fedha,Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5 Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA,Na kupata kumjua Mungu.
6 Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;