1 Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi;Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
2 Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba;Amkasirishaye huitendea dhambi nafsi yake.
3 Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake;Bali kila mpumbavu ataka kugombana.
4 Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi;Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.
5 Mashauri ya moyoni ni kama kilindi;Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka.
6 Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe;Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
7 Mwenye haki aendaye katika unyofu wake,Watoto wake wabarikiwa baada yake.