13 Usipende usingizi usije ukawa maskini;Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.
14 Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi;Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.
15 Dhahabu iko, na marijani tele;Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.
16 Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni;Mtoze rehani aliye mdhamini wa wageni.
17 Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu;Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe.
18 Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana;Na kwa shauri la akili fanya vita.
19 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.