16 Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni;Mtoze rehani aliye mdhamini wa wageni.
17 Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu;Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe.
18 Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana;Na kwa shauri la akili fanya vita.
19 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.
20 Amlaaniye babaye au mamaye,Taa yake itazimika katika giza kuu.
21 Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka,Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.
22 Usiseme, Mimi nitalipa mabaya;Mngojee BWANA, naye atakuokoa.