18 Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana;Na kwa shauri la akili fanya vita.
19 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.
20 Amlaaniye babaye au mamaye,Taa yake itazimika katika giza kuu.
21 Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka,Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.
22 Usiseme, Mimi nitalipa mabaya;Mngojee BWANA, naye atakuokoa.
23 Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa BWANA;Tena mizani ya hila si njema.
24 Mwenendo wa mtu watoka kwa BWANA;Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?