22 Usiseme, Mimi nitalipa mabaya;Mngojee BWANA, naye atakuokoa.
23 Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa BWANA;Tena mizani ya hila si njema.
24 Mwenendo wa mtu watoka kwa BWANA;Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?
25 Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu;Na baada ya kuweka nadhiri kuuliza-uliza habari.
26 Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki;Naye hulipitisha gurudumo la kupuria juu yao.
27 Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA;Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.
28 Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme,Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.