7 Mwenye haki aendaye katika unyofu wake,Watoto wake wabarikiwa baada yake.
8 Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu,Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake.
9 Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu;Nimetakasika dhambi yangu?
10 Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali,Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.
11 Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake;Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
12 Sikio lisikialo, na jicho lionalo,BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.
13 Usipende usingizi usije ukawa maskini;Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.