1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA;Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo.
2 Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huipima mioyo.
3 Kutenda haki na hukumuHumpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.
4 Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari,Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.
5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu;Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.
6 Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongoNi moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.
7 Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali;Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu.