12 Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya;Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia.
13 Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini,Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.
14 Kipawa cha siri hutuliza hasira;Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.
15 Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu;Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu.
16 Mtu aikosaye njia ya busaraAtakaa katika mkutano wao waliokufa.
17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
18 Mtu asiye haki ni fidia ya wenye haki;Naye afanyaye hila ni badala ya watu wa adili.