16 Mtu aikosaye njia ya busaraAtakaa katika mkutano wao waliokufa.
17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
18 Mtu asiye haki ni fidia ya wenye haki;Naye afanyaye hila ni badala ya watu wa adili.
19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika;Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
20 Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima;Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
21 Aandamaye haki na fadhili,Ataona uhai na haki na heshima.
22 Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu;Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.