19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika;Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
20 Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima;Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
21 Aandamaye haki na fadhili,Ataona uhai na haki na heshima.
22 Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu;Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.
23 Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake,Atajilinda nafsi yake na taabu.
24 Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi;Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
25 Matakwa yake mtu mvivu humfisha,Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.