1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi;Na neema kuliko fedha na dhahabu.
2 Tajiri na maskini hukutana pamoja;BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.
3 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
4 Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANANi utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
5 Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu;Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
6 Mlee mtoto katika njia impasayo,Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
7 Tajiri humtawala maskini,Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.