8 Yeye apandaye uovu atavuna msiba,Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma.
9 Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa;Maana huwapa maskini chakula chake.
10 Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka;Naam, fitina na fedheha zitakoma.
11 Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo;Mfalme atakuwa rafiki yake.
12 Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa;Bali huyapindua maneno ya mtu haini.
13 Mtu mvivu husema, Simba yuko nje;Nitauawa katika njia kuu.
14 Kinywa cha malaya ni shimo refu;Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.