11 Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu;Atawatetea juu yako.
12 Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho;Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.
13 Usimnyime mtoto wako mapigo;Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo,Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
15 Mwanangu, kama moyo wako una hekima,Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu;
16 Naam, viuno vyangu vitafurahi,Midomo yako inenapo maneno mema.
17 Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi;Bali mche BWANA mchana kutwa;