17 Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi;Bali mche BWANA mchana kutwa;
18 Maana bila shaka iko thawabu;Na tumaini lako halitabatilika.
19 Sikia, mwanangu, uwe na hekima,Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.
20 Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini,Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
22 Msikilize baba yako aliyekuzaa,Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
23 Inunue kweli, wala usiiuze;Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.