21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini,Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
22 Msikilize baba yako aliyekuzaa,Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
23 Inunue kweli, wala usiiuze;Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.
24 Baba yake mwenye haki atashangilia;Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.
25 Na wafurahi baba yako na mama yako;Na afurahi aliyekuzaa.
26 Mwanangu, nipe moyo wako;Macho yako yapendezwe na njia zangu.
27 Kwa maana kahaba ni shimo refu;Na malaya ni rima jembamba.