26 Mwanangu, nipe moyo wako;Macho yako yapendezwe na njia zangu.
27 Kwa maana kahaba ni shimo refu;Na malaya ni rima jembamba.
28 Naam, huotea kama mnyang’anyi;Huwaongeza wenye hila katika wanadamu.
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?Ni nani aliye na macho mekundu?
30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka;Huchoma kama fira.