31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka;Huchoma kama fira.
33 Macho yako yataona mambo mageni;Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.