4 Usijitaabishe ili kupata utajiri;Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.
5 Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu?Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa,Kama tai arukaye mbinguni.
6 Usile mkate wa mtu mwenye husuda;Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;
7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.Akuambia, Haya, kula, kunywa;Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
8 Tonge lile ulilokula utalitapika,Na maneno yako matamu yatakupotea.
9 Usiseme masikioni mwa mpumbavu;Maana atadharau hekima ya maneno yako.
10 Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani;Wala usiingie katika mashamba ya yatima;