6 Usile mkate wa mtu mwenye husuda;Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;
7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.Akuambia, Haya, kula, kunywa;Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
8 Tonge lile ulilokula utalitapika,Na maneno yako matamu yatakupotea.
9 Usiseme masikioni mwa mpumbavu;Maana atadharau hekima ya maneno yako.
10 Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani;Wala usiingie katika mashamba ya yatima;
11 Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu;Atawatetea juu yako.
12 Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho;Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.