13 Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema,Na sega la asali lililo tamu ulionjapo.
14 Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako;Ikiwa umekwisha kuiona;Ndipo itakapofuata thawabu;Wala tumaini lako halitabatilika.
15 Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki;Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
16 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena;Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
17 Usifurahi, adui yako aangukapo;Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
18 BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha;Akageuzia mbali naye hasira yake.
19 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya;Wala usiwahusudu wabaya;