19 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya;Wala usiwahusudu wabaya;
20 Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu;Taa ya mtu mbaya itazimika.
21 Mwanangu, mche BWANA, na mfalme;Wala usishirikiane na wenye kigeugeu;
22 Maana msiba wao utatokea kwa ghafula;Tena ni nani aujuaye uharibifu wa miaka yao.
23 Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili.Kupendelea watu katika hukumu si kwema.
24 Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki;Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia.
25 Bali kwao wakemeao furaha itakuwako;Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.