29 Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi;Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.
30 Nalipita karibu na shamba la mvivu,Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 Kumbe! Lote pia limemea miiba;Uso wake ulifunikwa kwa viwawi;Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana;Naliona, nikapata mafundisho.
33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!