4 Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwaVitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
5 Mtu mwenye hekima ana nguvu;Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo;
6 Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita;Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
7 Kwa mpumbavu hekima haipatikani;Hafumbui kinywa chake langoni.
8 Mtu afikiriye kutenda maovu,Watu watamwita mtundu;
9 Fikira za mpumbavu ni dhambi,Na mwenye mzaha huwachukiza watu.
10 Ukizimia siku ya taabu,Nguvu zako ni chache.