12 Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi;Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao;Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
14 Kama mawingu na upepo pasipo mvua;Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo.
15 Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa;Na ulimi laini huvunja mfupa.
16 Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;Usije ukashiba na kuitapika.
17 Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi;Asije akakukinai na kukuchukia.
18 Mtu amshuhudiaye jirani yake uongoNi nyundo, na upanga, na mshale mkali.