2 Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo;Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.
3 Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini;Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki.
4 Ondoa takataka katika fedha,Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;
5 Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme,Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki.
6 Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme;Wala usisimame mahali pa watu wakuu;
7 Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele;Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu.Yale uliyoyaona kwa macho,
8 Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania;Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye,Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.