8 Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania;Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye,Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.
9 Ujitetee na mwenzako peke yake;Bali usiifunue siri ya mtu mwingine;
10 Yeye asikiaye asije akakutukana;Na aibu yako isiondoke.
11 Neno linenwalo wakati wa kufaa,Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.
12 Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi;Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao;Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
14 Kama mawingu na upepo pasipo mvua;Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo.