1 Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno;Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.
2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
3 Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.
4 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Usije ukafanana naye.