17 Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake;Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.
18 Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge,Na mishale, na mauti;
19 Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake,Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?
20 Moto hufa kwa kukosa kuni;Na bila mchongezi fitina hukoma.
21 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka,Na kama kuni juu ya moto;Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.
22 Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo.Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
23 Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbayaNi kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.