23 Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbayaNi kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.
24 Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake;Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake.
25 Anenapo maneno mazuri usimsadiki;Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake.
26 Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila;Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.
27 Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe;Naye abingirishaye jiwe litamrudia.