15 Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi,Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;
16 Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo;Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta.
17 Chuma hunoa chuma;Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji;Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
20 Kuzimu na Uharibifu havishibi;Wala macho ya wanadamu hayashibi.
21 Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.