17 Chuma hunoa chuma;Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji;Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
20 Kuzimu na Uharibifu havishibi;Wala macho ya wanadamu hayashibi.
21 Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.
22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano;Upumbavu wake hautamtoka.
23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako;Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.