6 Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
7 Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali;Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
8 Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake;Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake.
9 Marhamu na manukato huufurahisha moyo;Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.
10 Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako,Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako.Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.
11 Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu;Ili nipate kumjibu anilaumuye.
12 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.