1 Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo,Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.
2 Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
3 Apendaye hekima humfurahisha babaye;Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.
4 Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu;Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
5 Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake,Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
6 Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya;Bali mwenye haki huimba na kufurahi.