12 Mwenye kutawala akisikiliza uongo;Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.
13 Maskini na mdhalimu hukutana pamoja;BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili.
14 Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu;Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
15 Fimbo na maonyo hutia hekima;Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
16 Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka;Bali wenye haki watayatazama maanguko yao.
17 Mrudi mwanao naye atakustarehesha;Naam, atakufurahisha nafsi yako.
18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia;Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.