19 Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno;Maana ajapoyafahamu hataitika.
20 Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno?Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
21 Amtunduiaye mtumwa wake tangu utoto,Mwisho wake atakuwa ni mwanawe.
22 Mtu wa hasira huchochea ugomvi;Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.
23 Kiburi cha mtu kitamshusha;Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
24 Mshiriki wa mwivi huichukia nafsi yake mwenyewe;Asikia maapizo, wala hana neno.
25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego;Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.