23 Kiburi cha mtu kitamshusha;Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
24 Mshiriki wa mwivi huichukia nafsi yake mwenyewe;Asikia maapizo, wala hana neno.
25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego;Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
26 Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu;Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA
27 Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki;Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.