7 Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini;Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue.
8 Watu wenye dharau huwasha mji moto;Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.
9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu;Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
10 Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu;Bali wenye haki humtunza nafsi yake.
11 Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote;Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
12 Mwenye kutawala akisikiliza uongo;Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.
13 Maskini na mdhalimu hukutana pamoja;BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili.