18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana;Ana heri kila mtu ashikamanaye naye.
19 Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi;Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
20 Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika;Na mawingu yadondoza umande.
21 Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako,Shika hekima kamili na busara.
22 Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako,Na neema shingoni mwako.
23 Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama,Wala mguu wako hautakwaa.
24 Ulalapo hutaona hofu;Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.