28 Usimwambie jirani yako,Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa;Nawe unacho kitu kile karibu nawe.
29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako,Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
30 Usishindane na mtu bila sababu,Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote.
31 Usimhusudu mtu mwenye jeuri,Wala usiichague mojawapo ya njia zake.
32 Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA,Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
33 Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu,Bali huibariki maskani ya mwenye haki.
34 Hakika yake huwadharau wenye dharau,Bali huwapa wanyenyekevu neema.