11 Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao;Wala hawambariki mama yao.
12 Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe;Ambao hawakuoshwa uchafu wao.
13 Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini!Na kope zao zimeinuka sana.
14 Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga;Na vigego vyao ni kama visu.Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
15 Mruba anao binti wawili,Waliao, Nipe! Nipe!Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe,Naam, vinne visivyosema, Basi!
16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa;Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!
17 Jicho la mtu amdhihakiye babaye,Na kudharau kumtii mamaye;Kunguru wa bondeni wataling’oa,Na vifaranga vya tai watalila.