23 Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo;Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.
24 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo;Lakini vina akili nyingi sana.
25 Chungu ni watu wasio na nguvu;Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
26 Wibari ni watu dhaifu;Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
27 Nzige hawana mfalme;Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
28 Mjusi hushika kwa mikono yake;Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
29 Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza,Naam, wanne walio na mwendo mzuri.