27 Nzige hawana mfalme;Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
28 Mjusi hushika kwa mikono yake;Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
29 Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza,Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote;Wala hajiepushi na aliye yote;
31 Jimbi aendaye tambo; na beberu;Na mfalme ambaye haasiki.
32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza;Au ikiwa umewaza mabaya;Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi;Na kupiga pua hutokeza damu;kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.