3 Wala sikujifunza hekima;Wala sina maarifa ya kumjua Mtakatifu.
4 Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini?Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake?Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake?Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi?Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
5 Kila neno la Mungu limehakikishwa;Yeye ni ngao yao wamwaminio.
6 Usiongeze neno katika maneno yake;Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
7 Mambo haya mawili nimekuomba;Usininyime [matatu] kabla sijafa.
8 Uniondolee ubatili na uongo;Usinipe umaskini wala utajiri;Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
9 Nisije nikashiba nikakukana,Nikasema, BWANA ni nani?Wala nisiwe maskini sana nikaiba,Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.